Somo 1. 2 Fal 25: 1-12
Ikiwa katika mwaka wa kenda wa kutawala kwake, katika mwezi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadreza mfalme wa Babeli, akaja yeye na jeshi lake lote, kipigana na Yerusalemu, akapanga hema zake kuukabili; nao wakajenga ngome juu yake pande zote. Basi mji huo ulihusuriwa hata mwaka wa kumi na moja wa mfalme Sedekia. Siku ya kenda ya mwezi wanne njaa ilikuwa nzito ndani ya mji, hata hapakuwa na chakula kwa watu wa nchi. Ndipo mahali pakabomolewa katika ukuta wa mji, watu wote wa vita wakakimbia kwa njia ya lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme; basi wa Wakaldayo walikuwa wakiuzuia mji pande zote; mfalme akaenda kwa njia ya Araba. Lakini jeshi la Wakaldayo wakamfuatia mfalme, wakampata katika nchi tambarare ya Yeriko; na jeshi lake lote walikuwa wametawanyika na kumwacha. Ndipo wakamkamata mfalme, wakamchukua kwa mfalme wa Babeli huko Ribla; wakatoa hukumu juu yake. Wakawauwa wana wa Sedekia mbele ya macho yake, wakampofusha macho Sedekia, wakamfunga kwa pingu, wakamchukua mpka Babeli. Hata mwezi wa tano, siku ya saba ya mwezi, ndio mwaka wa kumi na kenda wa mfalme Nebukadreza, mfalme wa Babeli. Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, mtumishi wa mfalme wa Babeli, akaingia Yerusalemu. Akaitelekeza nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto. Na jeshi lote la Wakaldayo, waliokuwa pamoja na huyo amiri wa askari walinzi, wakazibomoa kuta za Yerusalemu pande zote. Na mabaki ya watu waliosali katika mji, nao wale walioasi, na kumkimbilia mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu wote wengine, watu hao Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawachukua mateka. Lakini huyo amiri wa askari walinzi akawaacha watu walio maskini ili wawe watunza mizabibu na wakulima. |
Wimbo wa Katikati. Zab 137:1-6
1. Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, (K) Ulimi wangu ugandamane nisipokukumbuka. 2. Maana huko waliotuchukua mateka 3. Tuuimbaje wimbo wa Bwana 4. Ulimi wang una ugandamane |
Injili. Mt 8:1-4
Yesu aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata. Na tazama akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, “Bwana ukitaka, waweza kunitakasa. Yesu akanyoosha mkono, akamgusa, akasema, “Nataka; takasika.” Na mara ukoma wake ukatakasika. Yesu akamwambia, “Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako ukajioneshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.” |
TAFAKARI
IMANI YA KWELI INALETA UPONYAJI: Leo katika Injili tumesikia Yesu akimponya mtu mwenye ukoma. Ugonjwa huu ulikuwa tishio na wagonjwa wa ukoma walikimbiwa na watu na walitengwa wasikutane na watu. Tunaweza kuufananisha na ugonjwa wa korona jinsi wagonjwa walivyotengwa wasikutane na watu wengine. Mgonjwa huyu aliamini nguvu ya uponyaji iliyopo katika Yesu ndiyo maana alimwendea akaomba amponye. Yesu alipoona imani yake alimgusa kwa mkono wake na ukoma ukamwacha akapona akawa mzima. Kwa tendo hili Yesu alimpa uponyaji wa aina mbili kwani kwa kumgusa mwili wake alimponya dhidi ya ugonjwa wa upweke uliosababishwa na kutengwa na jamii, pili alimponya ukoma uliokuwa mwilini mwake. Wapendwa baadhi yetu ni wagonjwa wa maradhi mbalimbali. Baadhi tuna ukoma wa dhambi zinazotutenga na Mungu na Kanisa. Tumwendee Yesu atuponye tupatanishwe upya na Mungu kwa njia ya Sakramenti ya upatanisho. Tupatapo maradhi ya kimwili tusiende kwa waganga wa kienyeji bali tuende hospitali na Yesu atatuponya kupitia madaktari wake. SALA: Ee Yesu naomba uniongezee imani. |