Mzigo-TV-728x90

Masomo ya misa

Masomo ya Misa Agosti 2

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 02/08/2024

2024 AGOSTI 2: IJUMAA-JUMA LA 17 LA MWAKA

Mt. Eusebio wa Verseli, Askofu
Rangi: Nyeupe

Zaburi: Juma 1

Somo 1. Yer 26:1-9

Mwanzo wa kumiliki kwake Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hili lilitoka kwa Bwana, kusema, Bwana asema hivi, simama katika uwanja wa nyumba ya Bwana, useme na miji yote ya Yuda, wajao ili kuabudu katika nyumba ya Bwana; sema nao maneno yote ninayokuamuru kuwaambia, usizuie hata neno moja. Labda watasikia, na kughairi na kuacha kila mtu njia yake mbaya; ili niyaghairi mabaya niliyokusudia kuwatenda, kwa sababu ya uovu wa matendo yao. Nawe utawaambia, Bwana asema hivi, kama hamtaki kunisikia, kwenda katika sheria yangu, niliyoiweka mbele yenu, kuyasikiliza maneno ya watumishi wangu, manabii, ninaowatuma kwenu, naam, nikiondoka mapema na kuwatuma; lakini ninyi hamkuwasikiliza; basi, nitafanya nyumba hii kuwa kama Shilo, na mji huu nitaufanya kuwa laana kwa taifa zote za dunia. Na makuhani, na manabii, na watu wote, wakamsikia Yeremia, hapo aliposema maneno haya katika nyumba ya Bwana. Ikawa, Yeremia alipokuwa amekwisha kusema maneno yote ya Bwana aliyomwamuru kuwaambia watu wote, ndipo hao makuhani, na manabii, na watu wote, wakamkamata, wakisema, Bila shaka utakufa. Kwa nini umetabiri kwa jina la Bwana, ukisema, nyumba hii itakuwa kama Shilo, na mji huu utakuwa ukiwa, hautakaliwa na mtu? Watu wote wakamkusanyikia Yeremia katika nyumba ya Bwana.

Wimbo wa Katikati. Zab 69:5, 8-141

1. Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa change. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa Hodari, Adui zangukwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.   

(K) Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, ee Bwana.

2. Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu.     Na msikwao kwa wana wa mama yangu.    Maana wivu wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata. (K)

3.  Nami maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, Wakati ukupendezao; Ee Mungu,    Kwa wingi wa fadhila zako unjibu, Katika kweli ya wokovu wako. (K)

Injili. Mt 13: 54-58

Yesu alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii? Huyu si mwana wa Seremala? mamaye si yeye aitwae Mariamu? na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda? Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote? Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia, Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe. wala hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao. 

TAFAKARI

UNABII NI SAUTI YA MUNGU, TUISIKILIZE: Neno la Mungu linatuangaza kutambua mapendo ya Mungu kwetu. Anatupenda kiasi kwamba hapendi tuangamie kwa sababu ya maisha yetu mabaya. Amewatuma manabii ili kwa njia ya mafundisho yao, tuweze kujisahihisha na kuishi atakavyo Mungu. Jamii inayotaka kupotoka hujitenga na mapendo ya Mungu kwa kukataa neno lake hata na kuwatesa wale anaowatuma kutuonya. Kutokuishi atakavyo Mungu kutaifanya jamii yetu kuwa ukiwa, isiyo na mafanikio. Turudie maneno ya Mzaburi anayetualika akisema, “Ingekuwa heri leo msikie sauti yake, msiifanya migumu mioyo yenu (Zab 95:7 – 8).” Injili inatualika kutambua kuwa kushuka kwa imani kutatufanya tukose zawadi nyingi za kimungu ikiwa ni pamoja na uponyaji wa kweli, ambao hutoka kwa Mungu na kutujia kwa njia ya mwanaye Yesu Kristo. Wenyeji wa Nazareti wanatia shaka juu ya unabii wa Kristo na matokeo yake hawapati kile ambacho miji mingine walipata kutoka kwa Yesu. Hili ni onyo kwetu sisi pia kwamba tukiukataa ujumbe wa Mungu, tunamnyima Mungu nafasi ya kutenda ndani yetu.

Sala: Ee Mungu utujalie neema ya kuwapokea wajumbe unaowatuma kwetu.

About mzigotv

Recommended for you