Muziki-TV-728x90

Masomo ya misa

Msomo ya Misa Julai 29

By

on

Tumsifu Yesu Kristo. Karibu Katika Masomo ya Misa 28/07/2024

2024 JULAI 28: JUMATATU-JUMA LA 17 LA MWAKA

Mt. Marta

Rangi: Nyeupe
Zaburi: Juma 1

Somo 1. Yer 13:1-11

Bwana aliniambia hivi,”Enenda, ukajinunulie mshipi wa kitani, ukajivike viuno, wala usiutie majini.” Basi nikanunua mshipi sawasawa na neno la Bwana, nikajivika viunoni. Nalo neno la Bwana likanijia mara ya pili, kusema,”Twaa mshipi ule ulioununua, ulio viunoni mwako, kisha ondoka, enenda mpaka mto Frati, ukaufiche huko katika pango la jabali.” Basi nikaenda, nikauficha karibu na mto Frati, kama Bwana alivyoniamuru. Hata ikawa baada ya siku nyingi, Bwana akaniambia,”Ondoka, enenda mpaka mto Frati, ukautwae ule mshipi, niliokuamuru kuuficha huko.”Ndipo nikaenda mpaka mto Frati, nikachimba, nikautwaa ule mshipi katika mahali pale nilipouficha; na tazama, mshipi ulikuwa umeharibika, haukufaa tena kwa lolote. Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,”Bwana asema hivi, jinsi iyo hiyo nitakiharibu kiburi cha Yuda, na kiburi kikuu cha Yerusalemu. Watu hawa waovu, wanaokataa kusikiliza maneno yangu, wanaokwenda kwa ushupavu wa mioyo yao, na kufuata miungu mingine ile kuitumikia na kuiabudu, watakuwa hali moja na mshipi huu, usiofaa kwa lolole. Maana kama vile mshipi unavyoshikamana na viuno vya mtu, ndivyo nilivyowashikamanisha nami nyumba yote ya Israeli, na nyumba yote ya Yuda, asema Bwana; wapate kuwa watu kwangu mimi, na jina, na sifa, na utukufu; lakini hawakutaka kusikia.

Wimbo wa Katikati. Kumb 32:18-21

1. Hukumbuki Mwamba aliyekuzaa,
Mungu aliyekuzaa umemsahau.
Bwana akaona akawachukia,
Kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake.

(K) Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa.

2. Akasema, nitawaficha uso wangu,
Nitaona mwisho wao utakuwaje;
Maana, ni kizazi cha ukaidi mwingi,
Watoto wasio Imani ndani yao. (K)

3. Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu,
Wamenikasirisha kwa ubatili wao;
Nami nitawatia wivu kwa wasio watu.
Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo. (K)

Injili. Mt 13:31-35

Yesu aliwatolea mfano mwingine, akisema,”Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake. Nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake.”Akawaambia mfano mwingine;”Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia.”Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno; ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema: Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, nitayatamka yaliyositirika tangu awali.

TAFAKARI

TUONDOKANE NA UOVU TUMRUDIE MUNGU: Moja ya mbinu nzuri ya sala ni mtu anayesali aguswe na hiyo sala kabla haijamgusa Mungu. Kwa mfano mtu akae kwenye kiti atulie, atambua kuwa nguo zake zimeshikiliwa na mabega, miguu na mikono, atajisikia kiti kimeshikilia mwili na viatu vimeshikilia miguu. Tunapokuwa tumeguswa na sala sisi wenyewe tunajaribu kuwa tumemgusa Mungu kwa sala. Katika somo la kwanza Mungu anaeleza alivyoshikamana na nyumba yote ya Israeli, na nyumba yote ya Yuda. Maana kama vile mshipi ushikamanavyo na viuno vya mtu, ndivyo nilivyowashikamanisha nami asema Bwana. Lakini watu hawa wamekuwa waovu, wanaokataa kusikiliza maneno yangu, wanaokwenda kwa ushupavu wa mioyo yao, na kufuata miungu mingine ile kuitumikia na kuiabudu. Kwa sababu hizi Mungu anadhamiria kuwaharibu kwa sababu ya uovu. Lakini nabii Yeremia ametumwa kwao awaonye na awaalike wamrudie Mungu kwa toba. Ndio ujumbe tunaoupokea watu wa siku hizi za leo pia tumrudie Mungu tushikamane naye, sala yetu ituguse tusali tukiwa tumeshikamana na Mungu. 

Sala: Tunaomba bidii tuliyo nayo itusaidie kuzama kwenye uelewa wa upendo unaokukumbatia na kushikamana nawe.

 

About mzigotv

Recommended for you